EDUCATION

Mwanafunzi wa KCSE Afariki Dunia Akiwa Hospitalini Mombasa

Taarifa zinaonyesha kuwa marehemu, ambaye alikuwa anatoka Mombasa, alitafuta matibabu katika hospitali binafsi ya Bombolulu huko Kaloleni baada ya kuanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo, kabla hali yake kuzorota

Mwanafunzi anayefanya mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) katika Shule ya Upili ya St. George’s, eneo la Kaloleni, Kaunti ya Kilifi, amefariki dunia akipokea matibabu ya malaria

Kulingana na ripoti ya polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Mariakani, mwanafunzi huyo, anayejulikana kama Juma Mohamed, alifariki Alhamisi mchana katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Mariakani, ambako alikuwa amelazwa baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa malaria

Taarifa zinaonyesha kuwa marehemu, ambaye alikuwa anatoka Mombasa, alitafuta matibabu katika hospitali binafsi ya Bombolulu huko Kaloleni baada ya kuanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo, kabla hali yake kuzorota

Baadaye alikimbizwa Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Mariakani, ambako alifariki dunia akiwa bado anapokea matibabu

Akitibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Kaloleni, Adan Ibrahim, alisema mwili wa mwanafunzi huyo ulikuwa umehifadhiwa hospitalini humo na familia yake tayari imeuchukua kwa mazishi mjini Mombasa kulingana na desturi za Kiislamu

 Pia soma : Kaunti ya Nairobi Kuanza Ukaguzi wa Majengo Jumatatu, Wamiliki Wasiotii Sheria Kukabiliwa na Adhabu

Kifo hicho kimeshtua wengi huku maelfu ya watahiniwa kote nchini wakiendelea kufanya mitihani yao ya KCSE iliyonza rasmi Jumatatu wiki hii

Mwandishi : Mweru Mbugua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button