Wakili Nelson Havi Ajiuzulu Uanachama wa Chama cha UDA
Havi alitangaza uamuzi huo Ijumaa kupitia barua ya kujiuzulu aliyoiwasilisha kwa Katibu Mkuu wa chama hicho na nakala kutumwa kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa. Hata hivyo, hakutoa sababu za kuondoka kwake katika chama tawala
Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK), Nelson Havi, ametangaza rasmi kujiuzulu kwake kutoka Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kinachoongozwa na Rais William Ruto
Havi alitangaza uamuzi huo Ijumaa kupitia barua ya kujiuzulu aliyoiwasilisha kwa Katibu Mkuu wa chama hicho na nakala kutumwa kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa. Hata hivyo, hakutoa sababu za kuondoka kwake katika chama tawala
“Kwa mujibu wa Kifungu cha 14 cha Sheria ya Vyama vya Kisiasa, Cap 7D ya Sheria za Kenya, naomba kujiuzulu kama mwanachama wa United Democratic Alliance (UDA) kuanzia leo

Tafadhali mjulishe Msajili wa Vyama vya Kisiasa ili jina langu liondolewe katika orodha ya wanachama wa chama,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo ya tarehe 7 Novemba 2025
Havi alijiunga na UDA mwaka 2021 na kutangaza nia ya kuwania kiti cha Ubunge cha Westlands katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka uliofuata
Pia soma : Mwanafunzi wa KCSE Afariki Dunia Akiwa Hospitalini Mombasa
Wakati huo, alipokelewa na kiongozi wa chama William Ruto, aliyekuwa Naibu Rais, pamoja na viongozi wengine wa kisiasa
Mwandishi : Mweru Mbugua