Kaunti ya Nairobi Kuanza Ukaguzi wa Majengo Jumatatu, Wamiliki Wasiotii Sheria Kukabiliwa na Adhabu
Aliongeza kuwa agizo hilo linawahusu wamiliki wa mali, wapangaji, na mawakala wa usimamizi katika maeneo muhimu ya kibiashara kama CBD, Westlands, Upper Hill, Ngara, Kirinyaga Road na vituo vikuu vya manunuzi. Wanaokiuka masharti hayo wanaweza kuadhibiwa kwa kufungiwa biashara au kufikishwa mahakamani
Serikali ya Kaunti ya Jiji la Nairobi imepanga kuanza zoezi la ukaguzi wa majengo yote kuanzia Jumatatu ijayo, ili kuhakikisha yamehifadhiwa ipasavyo na kuzingatia viwango vya afya ya umma
Kwa mujibu wa Idara ya Afya na Lishe ya Kaunti hiyo, wamiliki wa majengo ambao hawajajenga upya au kupaka rangi majengo yao baada ya kupewa notisi ya mwisho ya siku 14 kutoka City Hall, watachukuliwa hatua za kisheria baada ya ukaguzi kufanyika
Waziri wa Kaunti wa Afya na Lishe, Bi. Suzanne Silantoi, alithibitisha kuwa maafisa wa idara yake wataanza ukaguzi huo rasmi Jumatatu
“Kuanzia Jumatatu, maafisa wetu wataanza ukaguzi wa kufuata masharti kwa majengo yoteyale yaliyopakwa rangi upya na yale ambayo bado hayajapakwa. Tulitoa muda wa siku 14, na ingawa wengi wameitikia, bado kuna wachache ambao hawajafanya hivyo,” alisema Silantoi

Aliongeza kuwa agizo hilo linawahusu wamiliki wa mali, wapangaji, na mawakala wa usimamizi katika maeneo muhimu ya kibiashara kama CBD, Westlands, Upper Hill, Ngara, Kirinyaga Road na vituo vikuu vya manunuzi. Wanaokiuka masharti hayo wanaweza kuadhibiwa kwa kufungiwa biashara au kufikishwa mahakamani
“Ni muhimu kurejesha hadhi ya Nairobi kama mji safi na wa kisasa wa Kiafrika. Hii ni mji mkuu, na lazima uakisi taswira hiyo kupitia majengo yake,” alisisitiza Silantoi
Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja, tayari amefuta ada zote za vibali vya upakaji rangi ili kupunguza mzigo wa kifedha kwa wamiliki wa mali
Pia soma : EACC Yashtaki Gavana Wamatangi na Wengine 13 kwa Ufisadi wa Zabuni wa KSh.813 Milioni
Agizo hilo linatokana na Sheria ya Afya ya Umma (Cap 242) na Sheria ya Mipango ya Ardhi na Matumizi (2019), ambazo zinahitaji majengo yote kufikia viwango vya chini vya matengenezo na afya ya umma
Silantoi alitaja baadhi ya majengo ambayo yamefuata agizo hilo, kama vile jengo la I&M, akiongeza kuwa mengine hayajapakwa rangi tangu yalipojengwa miongo kadhaa iliyopita
Wakazi wa Nairobi wanatarajiwa kushuhudia juhudi mpya za kurejesha mwonekano wa jiji na kulifanya liendelee kuwa mji wa kisasa wenye mandhari maridadi ya Kiafrika
Mwandishi : Mweru Mbugua




